Toleo 2026-10-29. Imesasishwa: 29 Oktoba 2026

Sera ya faragha

Sera hii inaeleza jinsi Mkononi360 inavyokusanya, kutumia, kuhifadhi na kulinda taarifa binafsi unapotumia tovuti yetu, apps zetu na kurasa zetu za umma. Tunafuata Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya mwaka 2022 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kanuni zake.

1. Sisi ni nani na jinsi ya kutufikia

Mkononi360 inaendeshwa na BVORTENIC TECHNOLOGIES, Tanzania. Kwa jambo lolote kuhusu taarifa zako binafsi, yakiwemo maombi na malalamiko, mhusika wetu wa ulinzi wa taarifa anapatikana kupitia [email protected].

2. Nafasi zetu mbili: mdhibiti na mchakataji

Mdhibiti: kwa akaunti yako mwenyewe (jina, email, simu, kumbukumbu za kuingia, subscriptions na malipo kwa Mkononi360) sisi ndio tunaoamua taarifa zinatumika kwa nini na vipi, kwa hiyo sisi ni mdhibiti wa taarifa.

Mchakataji: biashara na vikundi vinavyotumia apps zetu huweka taarifa za wateja wao, wapangaji, wanachama, wageni, wafanyakazi na wasambazaji. Kwa taarifa hizo biashara ndiyo mdhibiti na Mkononi360 ni mchakataji: tunazihifadhi na kuzichakata ili kutoa app tu, kwa maelekezo ya biashara. Maswali kuhusu taarifa hizo yaanze kwa biashara husika; tutaisaidia kujibu.

3. Taarifa tunazokusanya

Taarifa za akaunti: jina lako, email na namba ya simu, na tarehe uliyokubali masharti haya.

Taarifa za kuingia na usalama: codes za mara moja (zinahifadhiwa kama hash iliyolindwa tu), sessions, kifaa na browser unayotumia, anwani ya IP, na kumbukumbu za vitendo muhimu kwenye audit log.

Taarifa za app: unachoweka wewe au biashara yako kwenye app, kama mauzo na stoo, nyumba na wapangaji, ukodishaji, miradi, akiba na mikopo ya kikundi, miadi, mialiko, wageni na michango. Kila app inakusanya kile inachohitaji tu.

Kurasa za umma: mtu anapobook kwenye ukurasa wa biashara au kujibu mwaliko, tunakusanya jina na namba ya simu anayotoa, kwa ajili ya biashara hiyo.

Taarifa za malipo: ulicholipia, kiasi, njia na namba ya muamala kutoka kwa mtoa huduma wa pesa za simu. Hatuoni wala kuhifadhi PIN ya pesa za simu.

Cookies: angalia sehemu ya 9.

4. Kwa nini tunazitumia na misingi ya kisheria

Kufungua na kulinda akaunti yako na kukupa apps unazochagua (kutekeleza mkataba wetu nawe).

Kutuma ujumbe wa huduma kama codes za kuingia, risiti, vikumbusho ulivyoomba wewe au biashara, na taarifa kuhusu data yako (mkataba na maslahi halali).

Kuhifadhi kumbukumbu za fedha na usalama na kutimiza wajibu wa kisheria (wajibu wa kisheria).

Cookies za takwimu na ujumbe wa matangazo kwa ridhaa yako tu, ambayo unaweza kuiondoa wakati wowote.

5. Nani anapokea taarifa zako

Hatuuzi taarifa binafsi. Tunazishiriki na watoa huduma wanaotusaidia kuendesha Mkononi360 tu, chini ya masharti ya maandishi yanayowataka kuzilinda, au sheria inapotutaka:

Contabo: servers zetu na database zinaendeshwa kwenye servers zetu tunazokodi kutoka Contabo, ndani ya Umoja wa Ulaya.

Cloudinary: picha, logo na nyaraka unazopakia zinahifadhiwa na Cloudinary.

Brevo: barua pepe kama codes za kuingia na risiti zinatumwa kupitia Brevo, ndani ya Umoja wa Ulaya.

Tawk.to: chat ya moja kwa moja kwenye tovuti yetu, inapakiwa tu baada ya kukubali cookies za hiari au ukifungua chat mwenyewe.

Watoa huduma wa SMS na WhatsApp na watoa huduma wenye leseni wa pesa za simu, watakapounganishwa, kwa ajili ya kutuma ujumbe na kupokea malipo. Tutawataja kwenye sera hii kabla hawajapokea taarifa yoyote.

6. Taarifa zinazopelekwa nje ya Tanzania

Kwa sababu servers zetu ziko ndani ya Umoja wa Ulaya na baadhi ya watoa huduma wanafanya kazi nje ya nchi, taarifa zako binafsi zinahamishwa na kuhifadhiwa nje ya Tanzania. Tunafanya hivyo kwa watoa huduma wanaoweka ulinzi imara tu (usimbaji fiche wakati wa kusafirisha, udhibiti wa nani anafikia na masharti ya maandishi ya ulinzi wa taarifa), na kwa kufuata masharti ya Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kuhusu kuhamisha taarifa nje ya nchi.

7. Tunahifadhi taarifa kwa muda gani

Taarifa za app: zinahifadhiwa wakati subscription au majaribio ya app hiyo yanaendelea. Yakiisha na hayakuhuishwa, taarifa za app hiyo zinafutwa miezi 6 baadaye. Tunakutumia email siku 30 na siku 7 kabla.

Akaunti zisizotumika: akaunti isiyoingiwa kwa miezi 6 na isiyo na subscription inayoendelea inafutwa pamoja na taarifa zake zote. Tunakutumia email kabla; ukiingia inabaki.

Kumbukumbu za malipo: zinahifadhiwa kwa mwaka 1, kisha zinafutwa.

Mialiko: tukio, wageni wake na ujumbe wake vinafutwa siku 3 baada ya tarehe ya tukio.

Codes za kuingia, sessions zilizoisha, mialiko ya timu iliyoisha muda na kumbukumbu nyingine za kiufundi: zinafutwa zenyewe, kwa kawaida ndani ya siku chache.

Audit log: inahifadhiwa kama kumbukumbu ya usalama; akaunti ikifutwa inabaki na namba zisizomtambulisha mtu tu.

Ukifuta akaunti yako mwenyewe, vyote vilivyotajwa hapo juu vinafutwa mara moja.

8. Usalama

Tunalinda taarifa kwa usimbaji fiche wakati wa kusafirisha, kuingia bila password kwa codes za mara moja, kutenganisha taarifa za kila biashara ndani ya database, ruhusa kwa nafasi, vikomo dhidi ya matumizi mabaya na audit log. Wafanyakazi wetu wanafikia taarifa kwa kiwango kidogo na kinarekodiwa.

Taarifa binafsi zikivuja, tunarekodi tukio, tunachukua hatua kulidhibiti, na tunaiarifu Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi na watu walioathirika bila kuchelewa pale sheria inapotaka.

9. Cookies

Cookies muhimu zinakuweka umeingia kwenye apps zote za Mkononi360, zinakumbuka lugha na mwonekano, na zinalinda session yako. Zinakuwa zimewashwa daima.

Cookies za hiari (takwimu na chat ya Tawk.to) zinatumika tu ukizikubali. Chaguo lako linahifadhiwa, pia kwenye servers zetu kama ushahidi wa ridhaa, na unaweza kulibadilisha wakati wowote kupitia Mipangilio ya cookies chini ya tovuti.

10. Ujumbe

Ujumbe wa huduma (codes za kuingia, vikumbusho vya miadi na kodi, risiti) unatumwa kwa sababu ni sehemu ya huduma. Ujumbe wa matangazo, kama kampeni, maombi ya michango na shukrani, unatumwa kwa watu waliokubali kuupokea tu, hautumwi usiku, na kila mmoja unaeleza jinsi ya kujiondoa. Namba iliyoomba kujiondoa haipokei tena ujumbe wa matangazo kutoka app yoyote ya Mkononi360.

11. Haki zako

Una haki ya kupata taarifa zako (zipakue kwenye profile ya akaunti yako), kuzirekebisha (badilisha profile), kuzifuta (Danger Zone kwenye profile, au tuombe), kupinga uchakataji, kuondoa ridhaa, na kutuomba tupunguze uchakataji.

Kutuma ombi, tumia fomu ya maombi ya faragha kwenye ukurasa wa mawasiliano au tuandikie [email protected]. Tunajibu ndani ya siku 30.

Kama hujaridhika, una haki ya kulalamika kwa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya Tanzania.

12. Watoto

Akaunti za Mkononi360 ni za watu wenye umri wa miaka 18 au zaidi. Hatufungui akaunti za watoto kwa kujua.

13. Mabadiliko

Tukibadilisha sera hii tunasasisha toleo na tarehe hapo juu. Kwa mabadiliko muhimu utaombwa kusoma na kukubali toleo jipya utakapoingia tena.